Jifunze namna ya kutengeneza sabuni za maji na sabuni za miche, shampuu batiki, mishumaa na jinsi ya kuzingatia vipimo wakati wa kutengeneza sabuni
- Thread starterJumanne Mwita
- Start date
Jumanne Mwita
JF-Expert Member
Makala hii imeandaliwa kwa lengo la kumkwamua mjasiriamli katika kutengeneza bidhaa mbalimbali za ujasiriamali itumie kujigunza kunatengeneza bila kufundishwa.
Kupitia program maalumu ya mafunzo kwa njia ya mtandao, watu wengi sana wamenufaika kupitia blog hii na wengi wamebadilisha maisha yao kwa kujiajili kupitia mafunzo wanayoyapata huku.
Shuhuda nyingi ambazo zimetolewa na watu mbalimbali ni ushahidi tosha kuwa mafunzo haya yamewabadilisha sana.
Mafunzo haya ambayo hutolewa kwa njia ya mtandao huwekwa kwa lugha ya kiswahili na huwafikia watu walioko maeneo mbalimbali.
Mwaka 2017 moja ya mafunzo yaliyofanyika ni yale ambayo yalihusisha kujenga msingi wa mafanikio na unavyoweza kufanikiwa kifedha, mafunzo haya yalidumu kwa muda wa miezi 3. ni wengi walifanikiwa kupiga hatua na kutaka kuyapata mafunzo hayo kwa njia ya kitabu.
Yaliyomo humu ni kutoka kwenye Kijitabu katika sehemu ndogo ya mafunzo yaliyotolewa. Lengo ni kukupa maarifa ili nawe uweze kufanikiwa katika kuiishi ndoto yako.
Makala hii imeandikwa na Janeth James Mgongo (Mama Irene), ikiwa ni makala ya 2 Haki zote zipo chini ya Janeth James Mgongo. Haki zote zimehifadhiwa.
Huruhusiwi kunakili, kudurufu au kutumia sehemu ya makala hii bila idhini ya mwandishi. Kufanya hivyo itakuwa ni Ukiukwaji wa haki za mwandishi, na ukiukwaji wa taratibu. Hii unaweza kupelekea mashitaka toka kwa waandaaji wa kazi hii. Mpangilio wa ndani umefanywa na Jumanne Mwita.
YALIYOMO
UTANGULIZISEHEMU YA KWANZA
Mambo ya kuzingatia wakati wa kutengenezaSabuni
Sababu ya sabuni kujikata au kujitenga.
Vifaa vya usalama na vitendea kazi.
Kazi za malighafi.
Sabuni ya maji kanuni ya kwanza.
Sabuni ya maji kanuni ya pili.
Sabuni ya maji kanuni ya tatu
Sabuni ya maji kanuni ya nne
Sabuni ya maji ya caustic solution
Sabuni ya kuoshea vyombo
Sabuni ya chooni
PILI
Hair shampooShampoo ya alovera na asali
Shampooo ya tango
Shampoo ya alovera
Sabuni ya kunawia
Jiki za rangi
Jiki za kawaida
Sabuni ya maji ya kuogea
Window cleaner
Sabuni ya kuoshea magari
After shave
TATU
Mafuta ya mgandoMafuta ya kurefusha nywele
Mafuta ya mgando ya rika zote
Mafuta ya nazi ya mgando
Udi wa kuogea
Ubuyu wa vipande
Ubuyu wa Zanzibar
NNE
ChakiKanuni ya kuchanganya caustic soda na maji
Mold au vifyatulio vya sabuni
Sabuni za mche /kipande
Sabuni za magadi
Sabuni za magadi kanuni ya pili
TANO
Aina za batikiBatiki za kuchovya(tie and dye)
Batiki za mshumaa
Batiki za kublich
Batiki za kuprint
Batiki za kufinyanga
SITA
Sabuni ya ungaSiagi ya karanga
Body lotion
Lotion ya limao
Whitening & softening body serum
Coffee body scrub
Sugar scrub
Scrub yenye exfoliant zaid ya moja
SABA
Scrub isiyotumia majiScrub inayotumia maji
Kazi ya baadhi exfoliant
Tiles & sink cleaner
MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUTENGENEZA SABUNI
1. Vaa gloves ,mask na viatu vigumu kabla hautaanza kutengeneza sabuni2. Pima kemikali kwa kipimo maalumu usikadirie
3. Weka mbali na watoto kemikali
4. Weka chumba maalumu kemikali usiweke chumba cha kulala viumbe hai.
SABABU YA SABUNI KUJIKATA AU KUJITENGA
1. Kuzidi kwa chumvi2. Kuzidi kwa pafyumu
3. Uvivu wa kukoroga
4. Kupitwa kwa wakati kwa kemikali
5. Kuzidi kwa soda ash
Ili kuepuka tatizo hili fuata vipimo na taratibu zilizoelezwa kwenye makala hii.
VIFAA VYA USALAMA NA VITENDEA KAZI
VIFAA VYA MSINGI KATIKA UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA MAGADI NA TIBA
KIPIMIO
KAZI YA MALIGHAFI
SABUNI YA MAJI | ( kanuni ya kwanza )
Mahitaji
1. Sulphonic Acid -Lita 1 2. Sless -500g3. Soda Ash- 500g 4. Glycerine -250g
5. Cde -200g 6. Alka 2 _100g
7. Sodium Sulphate -300g 8. Rangi _2g
9. Perfume 50g 10. Maji_ 17.5
11. Dm dmh -40mls 12. Ph Inayotakiwa 6_8
Malighafi.
Hatua Za Utengenezaji
- Chukua ndoo weka sulphonic acid kwenye chombo cha kukorogea koroga soda ash light kwenye maji lita moja na nusu mimina kwenye sulphonic acid koroga
- Weka sless kwenye mchanganyiko wako anza kukoroga.
- Weka maji kidogo kidogo lita 10 lita kumi zilizobakia korogea alka tu kisha mimina kwenye ndoo yenye mchanganyiko ule wa mwanzo
- Weka Cde,Ongeza Glycerine Koroga
- Weka Rangi Na Perfume
- Weka Dm Dmh /Nu-Care
- Pima Ph
- Weka Kwenye Vifungashio Na Fungasha
UTENGENEZAJI WA SABUNI YA
MAJI (kanuni ya pili
MALIGHAFI1. Sulphonic acid -Lita moja
2. Siles au ungarol-lita moja
3. Soda ash-vijiko 15 vya chakula
4. CMC-VIJIKO 6 vya chakula
5. Maji Lita 30
6. Grisalini -vijiko 8
7. Pafyumu -kijiko 1-2 vya chakula
8. Rangi- kijiko kimoja
9. Chumvi ya mawe kilo moja Ila usiweke yote
10. Dm dmh –vijiko 5 vya chakula
Vifaa vya kutengenezea
1. Jaba au ndoo 2. Mwiko mkavu3. Gloves 4. Mask
5. Overral
Kuwa makini kuna baadhi ya kemikali hatari kwa afya
HATUA ZA UTENGENEZAJI WA SABUNI YA MAJI
1. Chukua ndoo au Jaba unaweka sulphonic acid Na Siles unakoroga kuelekea upande mmoja2. Weka soda ash Na cmc koroga kuelekea upande mmoja
3. Weka Maji Lita 30 koroga kuelekea upande mmoja kwa dakika 5
4. Weka grisalini,pafyumu Na rangi koroga kuelekea upande mmoja
5. Weka DM dmh na chumvi ambayo uliiloweka kwenye Maji weka kidogo kidogo huku ukipima uzito upendao ,ukishamaliza hapo funika Sabuni yako iache ipoe povu lote lishuke ndipo uanze kupaki kwenye Vifungashio
NB: Usiache bila kufunika pafyumu yako itaruka nakuisha kabisa.
SABUNI YA MAJI (kanuni 3)
MALIGHAFI1. Caustic soda solution-1ltr 2. Maji _20lita
3. Sulphonic acid_lita 2 4. Dm dmh-50 mls
5. Rangi ya Sabuni ya maji-5mls 6. Manukato -5mls
7. Chumvi gram 1000 ( usiweke yote )
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Chukua Kilo 1 Ya Caustic Soda Na Maji Lita 3 Koroga Kisha Ziache Zipoe Kwa Muda Wa Siku mbili2. Chukua sulphonic acid changanya na maji Lita 10 ukikoroga ongeza maji Lita 20
3. Koroga Hadi vipande vyeupe vitoweke Kisha weka chumvi ,rangi na manukato koroga kwa dakika 5
4. Pima kwa pH isome 6-8
5. Baada ya hapo weka kwenye vifungashio
SABUNI ZA MAJI (kanuni ya nne)
MalighafiMaji liter 30 au 40
1. Sulfonic acid 1 litre 2. Sles / Ungarol 1 litre
3 Soda ash light ½ kg 4. Gryceline ¼ litre
5. Ethanol 50ml 6. Cdea 50ml
7. Chumvi 1½ kg 8. Alka 2 /cmc 125 gram
9. Perfume 50ml 10. Rangi gram 5
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Andaa maji lita 40 chota Lita 3 kisha weka kando.2. Chukua sles tia ktk ndoo koroga tia chumvi kijiko kimoja kuyeyusha sless vizuri, koroga hadi upate cream Kama lotion iwe soft kabisa.
3. Chukua Sulfonic acid mimina ktk ndoo yenye sless kisha koroga vizuri na utie maji lita moja ili kulainisha mchanganyiko huo kisha koroga, ongeza soda ash ambayo uliiloweka ktk maji robo lita itie humo ktk mchanganyiko huo koroga vizuri ikianza kuleta ugumu anza kutia maji nusu Lita kisha koroga upate cream soft kabisa
4. Baada ya kupata cream soft endelea kutia maji lita moja moja hadi yaishe huku ukikoroga kuelekea upande mmoja pia maji tia upande katika ndoo na sio kumwagia katikati ya ndoo, ongeza chumvi kilo 1½ ile uliyoloweka koroga vizuri kabisa ilete uzito dakika 20
5. Baada ya kutia chumvi na kukoroga vizuri saana ( ukorogaji mzuri wa muda mrefu hufanya sabuni iwe nzuri na isiwe na wingu) ongeza cdea koroga.
6. Chukua alka 2/ cmc tia katika maji Lita 3 uliyotenga koroga vizuri upate uji mzito kisha miminia katika sabuni yako koroga vizuri kwa dakika 20 upate uzito zaidi ( usiloweke tigna na kuiacha itaganda na kuharibika.)
7. Tia gryceline kisha koroga,tia rangi kiasi ukitazama isizidi na kukolea saana, iwe rangi kiasi ili kuleta mvuto pia utakoroga kuelekea upande mmoja ili kuepusha povu kukuzuia kuona ndani, hii. ( Loweka rangi katika maji kiduchu ikoroge ndipo uitumie)
8. Tia ethanol 50ml na DM DMH Koroga vizuri Funika sabuni yako iache kwa iive kisha utaitia pafyum yako na kuifungasha tayari kwa matumizi.
UTENGENEZAJI WA SABUNI ZA MAJI
(kanuni 5)MALIGHAFI
1. Sless- ½ ( 500gm) 2. Sulphonic acid -1 kg
3. Caustic soda- 60gm 4. Soda ash- 125 gm
5. CMC/ALKA 2-80gm 6. Tigna- 250gm
7. Gryceline-250 ml 8. Ethanol- 50mls
9. Chumvi -500 g 10. Rangi-10gm
11. Perfume- 50mls 12. Maji -25
MAANDALIZI
1. Chukua caustic soda 60gm loweka katika maji ya 1000ml.2. Chukua soda ash 125gm loweka kwenye maji ya 1000mls.
3. Chukua Foaming booster 80gm loweka kwenye maji ya 1000mls
NB: Viache kwa muda wa masaa mawili.
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Chukua sless na sulphonic acid mimina kwenye jaba lako lisilo na maji kisha koroga kwa muda wa dk 5 hadi vichanganyike vizuri.2. Chukua caustic soda uliokuwa umeiloweka katika maji 1000mls mwaga katika mchanganyiko wa awali kisha koroga kwa muda wa dk 5
3. Chukua soda ash iliokuwa imelowekwa katika maji ya 1000mls mwaga katika mchanganyiko wako kisha endelea kukoroga kwa muda wa dk 3 hadi 5
4. Chukua booster iliokuwa imelowekwa kwenye maji ya 1000mls mwaga katika mchanganyiko wako wa awali kisha koroga vizuri kwa muda wa dk 5
5. Chukua Tigna ichanganye kwenye maji uliyo yaandaa 22000mls sawa na lita 22 ikologe kwa dk1 ichanganyikane vizuri kisha mimina hayo maji ambayo ni mchanganyiko na Tigna katika mchanganyiko wa awali.
Kisha utaendelea kukoroga mpaka pale utakapo ona uzito.
BAADA YA SABUNI KUWA NZITO.
6. Weka gryceline koroga kwa dk 17. Weka DM DMH/ethanol koroga kwa dk1
8. Weka industrial salt kisha koroga kwa dk 1
NOTE: Hapo sabuni yako itakuwa imekamilika kwa 90% kisha ifunike vizuri.
SIKU INAYOFUATA
1. Weka perfume kisha koroga kidgo2. Weka rangi kisha koroga kwa dk 3
NOTE: Baada ya hapo sabuni yako itakuwa tayari sasa kupeleka sokoni.
UTENGENEZAJI WA SABUNI YA MAJI MULTIPURPOSE KANUNI 5
Malighafi
1. Maji lita 25-302. Nitrosol 250
3. Ladi water lita 1
4. Sulphonic acid lita 1
5. Sless nusu lita
6. Dm Dmh mls 40
7. Pefume mls 50
8. Glycerine mls 100
JINSI YA UTENGENEZAJI
1. Chukua jaba weka maji kasha weka nitrosol koroga hadi iyeyuke
2. Weka ladi water kasha koroga weka sulphonic acid kisha koroga
3. Weka sles kasha koroga weka DM DMH koroga
4. Weka perfume,glycerine na rangi kasha koroga
5. Anza kuweka kwenye vifungashio tayari kwa kupeleka sokoni
DISINFECTANT LIQUID SOAP (Sabuni ya kudekia/kusafishia nyumba/chooni.
Hii ni aina ya sabuni ambayo hutumika kusafishia au kudekia mazingira ya nyumbani. Sabunii hii huuwa vijidudu (Germs) na Bacteria wazungukao sehemu za nyumba zetu, kama vile jikoni, chooni, sebuleni na maeneo mengine. Sabuni hii ni rahisi kutumia pia ni rafiki kwa matumizi ya nyumbani. Pia huondoa madoa au uchafu sugu kwa haraka zaidi.
MAHITAJI
1) LABSA/Sulphonic acid - ½ Lita 2) Maji – 19 Lita3) Boric acid – 100g 4) Borax – 100g
5) Rangi – 1Tbsp 6) Perfume(Lavender) – 100ml
7) Alka tu – 100g 8) Citric acid- 20g/
9) DM DMH-50MLS
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Weka maji lita 19 katika ndoo/Jaba kisha weka Alkatu 100g kisha koroga kwa dk 10 h adi 15.2. Ongeza Sulphonic acid ½ Lita kisha koroga vizuri.
3. Chukua Boric acid 100g na Borax 100g tia katika jagi lenye maji lita 1 koroga vizuri na kisha tia katika jaba letu endelea kukoroga kwa dakika 10.
4. Chukua rangi kiasi kidogo koroga pembeni katika maji kidogo, koroga vizuri kisha tia katika ndoo au Jaba la Sabuni na endelea kukoroga.
5. Weka DM DMH na endelea kukoroga.
Ongeza perfume ya Lemon/Dettol au Lavender 100ml kisha koroga vizuri na acha kwa saa 24 au zaidi kisha fungasha peleka sokoni.
HAIR SHAMPOO
Hii ni sabuni ambayo imebuniwa kwa ajili ya kusafishia nywele hata kama zimekaa muda mrefu bila kusafishwa. Hufanya nywele ziwe safi, huondoa uchafu na kuua wadudu walioko kwenye nywele na huondoa mba kwenye nywele. Hapa tutajifunza aina tofauti tofauti za shampoo zikiwemo zenye virutubisho vya matunda na mimea.
MAHITAJI /MALIGHAFI
1. Sless Lita moja na nusu 2. CDE-250 MLS3. Glycerine -500 MLS 4. Citric acid - 12 g
5. Rangi - 5gm 6. Perfume - 30-40 MLS
7. Maji Lita 20 8. Ph.5_ 7
9. DM DmH 40 MLS 10. Chumvi 300gm sio lazima
VIFAA
MZANI NDOO YA PLASTIKI
GLOVES MASKBUTI MWIKO WA KUKOROGEA
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Chukua ndoo weka sless peke yake KOROGA mpaka iwe kama cream ,weka maji kidogo kidogo mpaka yaishe huku ukiendelea kukoroga2. Weka CDE na glycerine KOROGA kwa dakika tatu
3. Weka citric acid ,pafyumu na rangi Kisha koroga vizuri kuelekea upande mmoja
4. Weka dawa ya kuzuia kuharibika DM DMH Kisha koroga vizuri kabisa Kama unatumia chumvi weka kidogo kidogo huku ukipima uzito unaouhitaji Kisha koroga
5. Pima pH 5_7 Kisha iache ipoe baada ya saa moja Anza kufungasha shampoo yako.
MAMBO YA KUZINGATIA
1. Koroga kuelekea upande mmoja.2. Rangi uweke kwenye maji hata nusu Lita Kisha Anza kuitumia
3. Katika kuboresha bidhaa yako unaweza kuongeza vionjo mbalimbali Ila lazima viwe vimefanyiwa utafiti
Mfano wa vionjo
Alovera, Asali, Tango, TangawiziPia viwe asilimia 2-5 Sawa na 200mls – 600mls
SHAMPOO YA ALOVERA NA ASALI
MAHITAJI /MALIGHAFIVIFAA
- Mzani
- Ndoo Ya Plastiki
- Gloves Mask
- Buti
- Mwiko Wa Kukorogea
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Chukua ndoo weka sless peke yake KOROGA mpaka iwe kama cream2. Weka maji kidogo kidogo mpaka yaishe huku ukiendelea kukoroga
3. Weka CDE na glycerine KOROGA kwa dakika tatu
4. Weka alovera na asali Kisha koroga vizuri
5. Weka citric acid ,pafyumu na rangi Kisha koroga vizuri kuelekea upande mmoja
6. Weka dawa ya kuzuia kuharibika DM DMH Kisha koroga vizuri kabisa Kama unatumia chumvi weka kidogo kidogo huku ukipima uzito unaouhitaji Kisha koroga
7. Pima pH 5_7 Kisha iache ipoe baada ya saa moja Anza kufungasha shampoo yako
SHAMPOO YA TANGO
MAHITAJI /MALIGHAFI1. Sless Lita moja na nusu 2. CDE-250 MLS
3. Glycerine -500 MLS 4. Citric acid - 12 g
5. Tango_600 MLS 6. Rangi - 5gm
7. Perfume - 30-40 MLS 8. Maji Lita 20
9. Ph.5_ 7 10. DM DmH 40 MLS
11. Chumvi 300gm sio lazima
VIFAA
Mzani, Ndoo Ya Plastiki, Gloves, Mask, Buti, Mwiko Wa Kukorogea
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Chukua ndoo weka sless peke yake koroga mpaka owe cream2. Weka maji kidogo kidogo mpaka yaishe huku ukiendelea kukoroga
3. Weka CDE na glycerine koroga kwa dakika tatu
4. Weka juisi ya tango Kisha koroga vizuri
5. Weka citric acid ,pafyumu na rangi Kisha koroga vizuri kuelekea upande mmoja
6. Weka dawa ya kuzuia kuharibika DM DMH Kisha koroga vizuri kabisa Kama unatumia chumvi weka kidogo kidogo huku ukipima uzito unaouhitaji Kisha koroga
7. Pima pH 5_7 Kisha iache ipoe baada ya saa moja Anza kufungasha shampoo yako
SHAMPOO YA ALOE VERA
Hii ni shampoo yenye virutubisho lishe vya aloe vera. Miongoni mwa vitamin zinazopatikana katika mmea huu ni vitamin B12 na B14 ambazo ni muhimu kwa ukuaji wa nywele. Hulainisha nywele kwa kuzuia ngozi kukauka, kuponya michubuko, kuzipatia nywele rangi yake na kuzuia nywele kujisokota.
MAHITAJI (LITA 10)
a) Maji -lita 10. b) Uice soft ya aloe vera -200ml.c) Cde -200ml. d) Gryceline – 100ml.
e) Sless –nusu lita f) Perfume – 20ml.
g) Rangi (kijani) –10ml h) Cmc/ akla 2 -100gm.
i) Dm dmh-50 mls. j) PH 5-7
JINSI YA KUTENGENEZA.
1. Pima maji lita 10 kwa kutumia measuring cylinder na mimina kwenye chombo cha kuchanganyia2. Chukua sless 1kg, gryceline 100ml, formaline 10ml, perfume 20ml na cde 200ml.Kisha vichanganye pembeni bila maji hadi vichanganyikane vizuri hadi sless iyeyuke kabisa.weka cmc/ alka 2 100gm kisha koroga tena vizuri hadi iyeyuke vizuri.
3. Weka juice yako ya aloe vera na koroga tena vizuri.
4. Malizia kwa kuweka rangi yako 10gm (kadiria) na weka DM DMH koroga tena hadi ishike vizuri.
5. Pima PH acha povu lishuke tayari kwa matumizi.
ANTI BACTERIAL HAND WASH/ SABUNI YA KUNAWIA
MAHITAJI1. Sless Lita 1 na nusu 2. Cde 250mls
3. Chumvi 500 gm 4. Glycerine 250 MLS
5. Rangi 5gm 6. Perfume-30had 40mls
7. Maji Lita 20 8. DM DMH MLS 40
10. IPA 50 MLS 11. Ph - 6-8
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Koroga slesa ponda ponda mpka iwe Kama cream2. Ongeza maji yenye chumvi (sodium sulphate) koroga
3. Weka cde koroga
4. Ongeza glycerine endelea kukoroga
5. Weka rangi koroga
6. Weka perfume ,ongeza DM DmH
7. Pima pH inatakiwa iwe 6-8,.Iache sabuni ishuke povu anza kufungasha.
DAWA YA MADOA KWA NGUO ZA RANGI.
Mahitaji.
1. Hydrogen peroxide 500- 1kg2. Chumvi 1kg
3. Soda ash 1kg
4. Culcium Hypoclorite 1kg
5. Maji 25L.
Utengenezaji
2. Tenga maji Lita 25 tia hypoclorite korogo iyeyuke yote, tia soda ash koroga dakika 103. Ongeza chumvi na hydrogen peroxide koroga vizuri funika acha kwa saa 24 kisha fungasha.
NB. Jaribu bidhaa yako kabla hujauza.
DAWA YA KUONDOA MADOA (jiki)
Malighafi
1. Maji lita 102. Breach//sodium hypochlorite nusu kilo
3. Soda ash-robo kilo
JINSI YA KUTENGENEZA
1. Mimina maji katika chombo cha kutengenezea weka breac/ sodium hypochlorite taratibu katika maji na ukoroge kwa dakika tano (5) ongeza soda ash na ukoroge kwa dakika 10 mpaka ichanganyike vizuri2. Acha ipoe kasha chuja weka kwenye vifungashio
SHOWER GEL(sabuni ya kuogea )
Hii ni Sabuni ya maji ambayo iko maalumu kwa ajili ya kuogea
MAHITAJI
1. Sless - kutakatisha na kuongeza povu
2. Cap b-kuongeza povu, inaongeza uzito na nzuri kwenye ngozi
3. Chumvi - uzito na kutunza
4. Glycerine -moisturizer
5. Citric acid -kuweka ph, vitamin C, kutunza
6. Rangi - mvuto
7. Perfume - harufu
8. Maji kibebeo Cha shower gel
9. Ph.kupima asid na base
10. Dm dmh - kutunza isiharibike
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Chukua chombo Cha plastiki WEKA siles koroga iponde ponder Hadi iwe Kama cream2. Weka maji yenye chumvi(chumvi koroga pembeni kwa kipimo kile like Cha sodium Sulphate)
3. Weka maji Lita mbili mbili huk u ukiendelea kukoroga kidogo kidogo
4. Weka Capb na endelea kukoroga
5. Weka Glycerine endelea kukoroga
6. Weka citric acid ,ongeza rangi na perfume alafu koroga
7. Weka Dm DmH Kisha koroga,pima pH iache ikitulia Anza kuweka kwenye vifungashio
Mambo ya kuzingatia
1. Inashauriwa pafyumu isowe Kali Sana iwe imepoa2. Unaweza kuweka vionjo ili kufanya ipendeze na kuteka soko
3. Unaweza kuweka matunda ,Castro Oil, Olive Oil
Vitu hivi viwe vimefanyiwa utafiti na kujiridhisha na sababu za kuviweka
4. Usisahau kuweka preservative ili shower gel isioze
5. Kama unaweka malighafi za mafuta Ni vizuri kuweka emulsifier mf polysobate
Kama unaweka malighafi za mafuta ratio iwe 2% Hadi 5% sawa MLS 200 Hadi 600mls
WINDOW & GLASS CLEANER
Hii ni bidhaa ambayo hutumika kwa matumizi ya kusafishia vioo na vyombo mbalimbali aina ya glass. Huenda vioo vya madirisha au magari, watu wengi huwa wanamiliki vitu ambavyo vina material ya vioo na hawajui jinsi gani ya kusafisha hivyo vioo punde baada ya kuchafuka.Hii ni bidhaa nzuri ambayo mara nyingi hutumika katika kusafishia madirisha ya vioo au kifaa chochote ambacho kimetengenezwa kwa material ya kioo,
MALIGHAFI ZITUMIKAZO KATIKA KUTENGENEZA
WINDOWS CLEANER1. Sabuni ya maji
2. Vinegar ( ACETIC GRACIAL ACID )
3. Maji safi
JINSI YA KITENGENEZA WINDOWS CLEANER
1. Utakuwa na maji lita kumi kama unataka kutengeneza lita kumi.Chukua sabuni yako lita moja kisha mimina katika chonbo chako ulicho aandaa ili utengeneze windows cleaner.2. Chukua vinegar ( acetic gracial acid ) lita moja kisha uta mimina katikas chombo ambacho uliweka sabuni yako ya maji.. Kisha utakoroga mpaka utakapoona kuwa imekuwa vzuri kabisa. So povu litatokea jingi sana so unaweza ukaicha kwa kipindi flani hivi ( takribani dakika 5 ) mpaka utakapoona kuwa povu limetoka loteee.
Na hapo inakuwa umeweza kutengeneza windows cleaner kwa njia nyepesi kabisa.
SABUNI YA KUOSHEA MAGARI
Sabuni ya maji ya ya kuoshea magari ni moja ya sabuni pendwa sana mijini kutokana na urahisishaji wake ktk kuoshea magari pamoja na ubora wake.Sabuni ya maji ya kuoshea magari haipaswi kuwa na kemikali ili isipaushe magari na kupoteza ule mng'ao wa magari.Sabuni hii itaacha gari yako ktk mng'ao mzuri sana, pia haitapauka kutokana na malighafi hizi ambazo hazina kemikali.
Mahitaji:
1. Sless/ ungarol 1½kg =2. Cocamidopropyl betaine ¼L
3. Isopropyl Alcohol/ Ethanol 200ml
4. Grycleline ¼L
5. Coconut oil 100ml
6. Perfume 25ml
7. Color 20g
8. Salt 100g
9. Tigna/CMC 125g
10. Maji 20L.
KAZI ZA MALIGHAFI
1. Sles -Kuweka povu, kuondoa uchafu, kuweka utelezi.2. Cocamidopropyl betaine - Kuongea povu, utelezi, mng'ao wa sabuni na ulaini/ smoothly.
3. Isopropyl Alcohol/ Ethanol -Kitunza sabuni, husaidia kulegeza uchafu mgumu utoke.
4. Grycelin-Huleta ulaini, utelezi, huzuia gari isipauke.( Mafuta)
5. Coconut oil-Hulainisha sabuni, huacha gari ktk hali ya unyevu unyevu isipauke na kuwa kavu.
6. Pafyum- Harufu
7. Rangi -Muonekano.
8. Tigna /CMC-Uzito, povu, utelezi.
9. Chumvi- imetumika kusaida kuyeyusha sless, pia kutunza sabuni & kuongezea uzito.
10. Maji 20L.
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Pima sless 1½ kg ktk jaba/ ndoo yako, tia chumvi 100g pamoja koroga kwa dakika 20 upate rojo laini kama lotion.2. Tia maji Lita 4 koroga dakika 15 kuelekea upande mmoja, ongeza maji Lita 6 koroga dakika 15.
3. Ongeza maji lita 7 koroga dakika 15- 20.
4. Tia Grycelin koroga dkk 3, ongeza cdea koroga dkk 15.
5. Tia coconut oil koroga dkk 3, ongeza Isopropyl Alcohol/ Ethanol koroga dakika 5.
6. Tenga maji Lita 3 yaliyobakia, tia tigna koroga upate uji mzito, tia kaika sabuni yako koroga dkk 15 funika acha kwa saa 24.
7. Baada ya saa 24 tia pafyum 25ml koroga dkk 5
8. Tia rangi 20g iliyoloa maji koroga dkk10 kisha fungasha tayari kwa matumizi.
Mtaji Tsh 24,000/= tu, sabuni Lita moja Tsh 3,000/=
AFTER SHAVE
MAHITAJI1. Ethanol- 200ml 2. Glycerine- 50ml
3. Menthol- 1tbsp 4. Colour
5. Perfume- 10ml
UTENGENEZAJI
1. Pima kiasi cha Ethanol na uyeyushe Menthol ndani ya chombe chenye Ethanol.2. Koroga vizuri mchanganyiko huo.
3. Ongeza Glycerine na ukoroge.
4. Ongeza tena Ethanol katika mchanganyiko wako na ukoroge tena vizuri.Ongeza perfume na rangi kisha koroga vizuri.After shave itakuwa tayari kwa matumizi.
MATUMIZI: hutumika baada ya kunyoa(ku shave). mfano ukisha nyoa ndevu una paka hii after shave kuzuia kutokwa na vidonda au mapele.
MAFUTA YA MGANDO
Mafuta ya mgando ni mojawapo ya vilainishi vya ngozi vinavyoipa ngozi mwonekano wa kuvutia na nyororo.
Mahitaji.
1) Micro wax 0.5kg.2) White oil 0.5 Lita.
3) Glycerine ya kiwandani 20ml.
4) Perfume 25ml.
5) Rangi tone mbili.
6) Jiko lenye moto.
7) Sufuria.
8) Vifungashio.
Jinsi ya kutengeneza
1. Washa jiko lako moto kiasi na ubandike sufuria.2. Weka micro wax nusu kilo ndani ya sufuria na subiri iyeyuke.
3. Weka white oil nusu Lita na koroga vizuri.
4. Weka perfume 25ml. na koroga tena.
5. Shusha mafuta yako na subiri yapoe kiasi {usiache yakapoa sana }
6. Malizia kwa kuweka glycerin yako 20ml{mafuta yakiwa chini} kisha koroga tena vizuri.
7. Weka kwenye vifungashio tayari kwa matumizi.
NB: Mafuta haya yanaviwango vya TBS hivyo yafaa kwa matumizi ya watu wa rika na jinsia zote {Mtoto mdogo hadi mzee }
Mtaji wa mafuta ya mgando Lita 1.
1. Microwax ½ kg Tsh 3000/=2. White oil ½ kg Tsh 3000/=
3. Grycelin ¼ litre Tsh 1500/= tumia 20ml tu.
4. Perfume 50ml Tsh 3,000/= tumia 10ml tu.
5. Rangi (optional) Tsh 1000/= tumia tone 2.
Jumla Tsh 11,500/= tu
Utatoa mafuta 1000ml sawa na vichupa 20 vya 50ml kila kichupa uza Tsh 1,500 hadi 2000, vifaa kama Grycelin, rangi, pafyum, vitabaki.
MAFUTA YA KUREFUSHA NYWELE
1. White Oil 1 lita2. Micro Wax 1 lita
3. Olive Oil vijiko 11 vya chakula
4. Castrol Oil ½lita
5. Majani ya Mvuje 10
6. Majani ya Rosemary Kichane 1
7. vitunguu Swaumu 6 punje
8. Vitunguu maji 3 vyekundu
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Yeyusha White Oil+Micro Wax kwa njia ya double boil.Ikiyeyuka weka Castrol Oil na uipue.2. Chemsha Olive Oil Vijiko 6+Vitunguu swaumu+Vitunguu maji (Unaweza kusaga kabla) Kisha chuja na uchanganye kwenye mchanganyiko wa Awali.
3. Chukua tena Olive Oil Vijiko 5+Mvuje +Rosemary Chemsha Kisha uchuje na uchanganye kwenye mchanganyiko wa Awali.Koroga vyema.
4. Weka Rangi ya Mafuta (Kijani/njano hupendeza zaidi) Weka Perfume, koroga. Yakipoa mimina katika package ulizoziandaa yaache yagande Kisha tayari kwa matumizi.
MAFUTA YA MGANDO KWA RIKA ZOTE(WATOTO HADI WAZEE)
MAHITAJI1. White oil - 2 lita
2. Micro wax - 1 kg
3. Pure coconut oil -¼ lita
4. Gryceline - 50mls
5. Perfumu (sio lazima)- 25ml
6.Rangi (sio lazima) - tone 2
7. Aloe vera gelly - 200mls.
VIFAA
Jiko lenye moto, SufuriaIfungashio, Mwiko/kijiko cha kukorogea
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Washa jiko lako moto na ubandike sufuria.2. Weka micro wax ndani ya sufuria na subiri iyeyuke,Kisha weka white oil lita 2 na koroga vizuri.Kisha ongeza coconut oil na Aloe vera gelly kisha koroga vizuri.
3. Weka Gryceline na uendelee kukoroga, weka perfume na koroga tena.Shusha mafuta yako na subiri yapoe (usiache yakapoa sana kwani yataganda kabla hujaweka kwenye vifungashio)
4. Weka kwenye vifungashio tayari kwa matumizi.
NB: Mafuta haya yanafaa kwa matumizi ya watu wa rika na jinsia zote.(watoto hadi wazee)
MAFUTA YA NAZI YA MGANDO
Mahitaji
1. White Oil 1 litre2. Micro Wax 1 Litre
3. Pure Coconut Oil ¼ litre
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Chukua sufuria weka jiko weka maji chukua nyingine ndogo kwa kutumia njia ya double boil,Weka vyote jikoni viyeyuke.2. Vikishayeyuka na kuchanganyikana,ipua na uache yapoe.Yakishapoa mimina katika package ulizoziandaa yagande Kisha tayari kwa matumizi.
NB. Haya anaweza kutumia mtoto wa kuanzia miaka miwili na kuendelea.
UDI WA KUOGEA
UDI huu hutumika kuweka kwenye maji ya kuogea.Maji yanakuwa na harufu nzuri mno, badala ya kuweka hiriki, au mchaichai weka Udi unukie siku nzima.MAHITAJI
1. Soap base (Transparent) - 120g2. Cocoa butter- 30ml
3. Essential oil- 15ml
4. Rangi- 5ml/kijiko cha chai.
JINSI YA KUTENGENEZA
1. Weka sufuria jikoni kisha weka vipande vya soap base na cocoa butter na acha viyeyuke.2. Vikisha yeyuka zima jiko.
3. Weka essential oil ( perfume) na changanya vizuri.
4. Kama utahitaji kuweka rangi zaidi ya moja basi gawa mchanganyiko wako kila mmoja weka rangi unayotaka.
5. Mimina kwenye mold kugandisha
6. Kwa muda wa saa 24 na kuendelea zitakuwa zimeshaganda.
7. Pack kwenye vifungashio vyako tayari kwa matumizi.
NB: Kikopo huuzwa Tsh.1000 I nategemeana na eneo ulilopo.
UTENGENZAJI WA UBUYU WA VIPANDE
Mahitaji
1. Unga wa Ubuyu -kilo moja2. Sukari-kilo moja Na nusu
3. Radha-nusu kijiko cha chakula
4. Rangi-vijiko 2-3
5. Maji –nusu Lita
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Chemsha Maji jikoni weka sukari koroga mpakaiyeyuke kisha weka radha Na rangi koroga2. Uache mkorogo wako uchemke had uanze kunata nata anza kuweka unga wa Ubuyu huku ukisonga kama ugali Na kuzidi kuongeza unga mpaka uishe
3. Ukisha changanyika vizuri anza kumimina kwenye chombo cha plastiki ulichoanza kupaka mafuta ya kula ili usigande ukikauka tandaza vizuri kisha uache ukauke
4. Ukikauka anza kukata vipande uvitakavyo wewe kwa ajili ya kuuza au kula
NB: weka maji zaidi ya robo lita kwa ajili ya akiba kama maji yatakuwa machache unaweka ya akiba hayo.
UBUYU
MAHITAJI1. Sukari vikombe 2
2. Maji vikombe 2
3. Nusu kikombe unga wa ubuyu
4. Vikombe 4 ubuyu wenyewe
5. Kijiko ¼ cha pili pili ya unga
6. Kijiko ¼ cha chumvi
7. Kijiko ¼ cha iliki ya unga
8. Rangi nyekundu au yeyote utakavyopenda.
JINSI YA KUPIKA
1. Katika sufuria, weka maji na sukari na chumvi na pili pili ya unga na Rangi na iliki. Moto uwe juu kiasi na changanya vyote hivyo vipike vizuri.2. Wakati vitu vinaanza kujipika utakuta rojo linatoa mapovu. Endelea tu kukoroga acha rojo lipikike vizuri. Baada ya hapo mapovu yakianza kutulia inamaanisha kua rojo limeanza kua zito. Sasa hapo chota kidogo katika mwiko na test kwa vidole kama rojo linanata ua halinati. Rojo linatakiwa linate ndio linakua limeiva. Lisinate Sana kiasi tu.
3. Kisha mimina ubuyu wa kokwa na changanya vizuri kabisa katika rojo. Endelea kupika vizuri kama dakika 2 hivi. Kisha mimina unga wa ubuyu na changanya vizuri tena.
4. Endelea kupika mpaka unaona sukari inaanza kuganda na kung'aa na kushika vizuri katika ubuyu.
5. Hapo sasa zima jiko na mimina ubuyu katika sinia kubwa na acha ubuyu upoe.
CHAKI
Chalk ni bidhaa ambayo imebuniwa kwa ajili ya matumizi ya shule, vyuo n.kChalk zinatofautiana kutokana na malighafi inayotumika, Rangi aina ya chokaa, Gypsum iliyotumika kutengenezea Isiyo na dust
(dustless)
CHALK No.1
Chalk ambayo malighafi yake ni CHOKAA.
Malighafi
1. Chokaa nyeupe 1kg2. Maji 1lita
3. Rangi kama unahitaji iwe ya rangi
4. Foil paper (mould)
5. Moto.
6. PLASTER OF PARIS (P.O.P)
Hii ni malighafi muhimu sana, na ndio malighafi kubwa inayotakiwa kwa kiwango kikubwa sana katika utengenezaji wa chaki hizo tunazozizungumzia. Kitaalamu au kisayansi zinaitwa “Calcium carbonate”. Hii inatengeneza uji mzito na kukauka kwa haraka sana pale inapochanganywa na maji. Mbali na kutengeneza chaki, inatumika hospitalini kutengenezea muhogo (Kiswahili cha mtaani) kuzunguka mguu au mkono uliovunjika
HATUA ZA KUTENGENEZA
1. Chokaa kilo moja na iwe imechekechwa na kupata unga ulio safi, Maji lita moja, Rangi ya chakula 10 mls.Mchanganyiko huu uchanganywe kwa pamoja na upate uji mzito, koroga kwa muda wa dakika 15.2. Weka mchanganyiko wako katika mould ya fowl paper zikate ziwe na shape ya saizi ya chaki unayotaka ,Weka juani chaki zako mpaka zikauke Zikikauka, toa kwenye foil paper tuziingize jikoni kama tunavyochoma vyungu na matofali ili kuhahakikisha imeiva ukiishika inaacha vumbi mkononi na ikidondoka inakatika vipande vingi.
KANUNI ZA KUCHANGANYA CAUSTIC SODA NA MAJI KWA USAHIHI
KANUNI YA KWANZA
1. Caustic Soda Kilo 25 Maji Lita 802. Caustic Soda Solution Lita 10 Mafuta Lita 20
Kama Unatumia Hydrometer Unapima Baume 30
KANUNI YA PILI KWA VIPIMO VIDOGO 1.CAUSTIC SODA KILO MOJA MAJI LITA 3
CAUSTIC SOLUTION LITA MOJA MAFUTA LITA 2
Kwa kutumbukiza hyrometer kwenye caustic solution tupate baume 30 kama itakuwa imepungua ongezaCaustic soda kisha koroga kupima tena kama imezidi ongeza maji kisha pima tena
NB: Vipimo hivi kwa wanaotumia hydrometer hata wale wasiotumia hydrometer wanatumia kutengeneza sabuni.
MOLD NA VIFYATULIO VYA SABUNI
- Kuna mold za aina nyingi zipo za chuma ambazo ukihitaji kumwagia mchanganyiko wako unapaka grisi.
- Kuna mold za mbao ambazo ziko ndogo kwa ajili sabuni za tiba za vipande pia zipo kubwa za sabuni ya mche au magadi
- Pia aina ya tatu kuna mold zinaitwa silicon mold kwa ajili ya sabuni za tiba za kuogea
Namna ya kudesign mold inategemea na vipimo vyako vya sabuni ambayo unataka iwe
Mfano mold ya sabuni za magadi urefu wa mche huo ndio uwe upana wa mold urefu na kimo unakadiria ila upana tu uwe unafanana na mche wa sabuni ambao ulionao kama sampo.
Mfano wa mold mbalimbali
SABUNI ZA MCHE/KIPANDE
MAHITAJI1. Mafuta Lita 20 (mawese,mise)
2. Caustic solution Lita Lita 10
3. Sodium silicate robo Lita
4. Rangi gram 25-30 sio lazima
5. Pafyumu MLS 50 sio lazima
Mfano wa sabuni ya mche
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Vaaa gloves chukua chombo Cha plastic weka mafuta na pia chukua ndoo weka caustic solution changanya na sodium silicate koroga ukimaliza2. Chukua mchanganyiko wenye caustic solution + sodium' silicate nenda kaweke kidogo kidogo kwenye mafuta huku ukiendelea kukoroga weka rangi na pafyumu koroga
3. Kama unatumia mold ya chuma weka grisi kwenye mold au Kama unatumia mold ya mbao weka nailoni Anza kumwagia mchanganyiko wako na uache uakuke kwa masaaa kadhaa ukikauka Anza kukata tayari kwa kupelekea sokoni.
JEDWALI LA KANUNI
SABUNI ZA MAGADI (gwanji)
Ni moja ya sabuni ambazo zinapendwa Sana na kuweza kuteka soko kwa kiasi kikubwa sana.MAHITAJI
1. Mafuta ya mise Lita 202. Caustic solution Lita 10
3. Sodium silicate robo Lita
4. Rangi ya Sabuni 30 gram
Mfano wa sabuni ya Magadi
HATUA ZA UTENGENEZAJI
Mafuta Caustic Sodium Rangisolution silicate
1 Lita 5 Lita 2.5 Mls 50 5 gm
2 Lita 10 Lita 5 Mls 100 10 gm
3 Lita 20 Lita 10 Mls 200 20 gm
4 Lita 40 Lita 20 Mls 400 40 gm
1. CHUKUA NDOO YA PLASTIKI WEKA MAFUTA PIA
Chukua ndoo nyingine Pima caustic solution Lita 10 yenye BAUME 302. Chukua caustic solution weka sodium' silicate kuroga kwa muda wa dakika 2-3 ukimaliza Anza kumimikia mchanganyiko wa caustic solution na sodium silicate kwenye mafuta huku ukiwa unakoroga koroga kwa muda Hadi mchanganyiko uchanganyike vizuri
3. Chota uji wako kiasi Kama Lita mbili Hadi tatu weka pemben Pima rangi yako Anza kuchanganya na uji ule mdogo ulioutenga pembeni.
4. Chukia mchanganyiko wako mweupe Anza kumimina kwenye kibao Cha kufyatulia kidogo na Kisha unamimina wa rangi ya bluu kiasi unakuwa unafanya hivyo Hadi mchanganyiko wako wote uishe wa bluu na mweupe uki maliza chukua mti anza kuchoza zig zag au nane juu ya kibao Cha kufyatulia ukimaliza acha ukauke
5. Ukikauka Anza kukata sabuni yako kwa kufuata ukubwa ambao utakuwa unauhitaji
SABUNI ZA MAGADI
MAHITAJI1. Caustic Soda kilo 3 na gram 400
2. Mafuta ya mise lita 20
3. Sodium Silicate robo Lita
4. Maji lita 10
5. Rangi ya bluu vijiko 3
6. Mold ya kufuatilia
Jinsi ya kutengeneza
1. Pima maji Lita 10 Weka Caustic soda 3kg na gram 400 kwenye maji yako Lita 10 kisha koroga vizuri hadi iyeyuke iache kwa masaa 24.2. Chukua caustic solution yako uliyoikoroga kiasi cha 10 lita weka sodium silicate koroga kuelekea upande mmoja.
3. Pima mafuta ya mise/mbosa 20 lita na mimina kwenye caustic solution yako kisha koroga vizuri. Na haraka haraka.
4. Chota huo uji kiasi ( lita 2 hadi 3} kisha weka rangi yako kwenye ule uji uliouchota pembeni na koroga vizuri hadi rangi ikolee.
5. Mimina kiasi chako cha uji usio na rangi kwenye mold au box la kugandishia.Anza kumimina uji wako wenye rangi pembeni ya mold/box lako la kugandishia kuzunguka.
6. Chukua mti wako wa kukorogea na chora namba 8 kwenye uji wako ulioumimina kwenye mold au box kwa kutumia mti wako wa kuchanganyia hadi yatokee mawimbi ya rangi yako.
NB: Hifadhi uji wako sehemu yenye kivuli na uache wazi ili ugande.sabuni yako inakauka baada ya masaa 4 hadi 6 tayari kwa kukata.
BATIKI ZA AINA MBALIMBALI
Batiki ni nini?
Ni nguo au kitambaa cha pamba asilimia 100 kilichotiwa rangi kwa kuchora, kugonga, kuchovya, kunyunyiza au kuchubua.
Historia ya Batiki.
Batiki ilikua kama vazi lililoundwa au kubuniwa nchi za China na India, lakini kutokana na ukuaji na technolojia inavyozidi kukua ikasambaa mpaka kuingia hapa nchini kwetu na kushika hatamu. Hivi inavyokwenda wabunifu wengi wameweza kubuni kila aina ya mitindo mpaka kuipa sifa ya kuingia katika mitindo maalum ya Kitaifa.Ili iwe batiki lazima kuwe na aina fulani ya muundo bila hivyo itasomeka ni nguo ya kawaida tu.Batiki hutengenezwa kwa kutumia malighafi kadhaa.Malighafi hizi zote ni hatari na zinatakiwa kutumiwa na kutunzwa kwa uangalifu na mtu anaetumia basi lazima azijue hatari na jinsi ya kujilinda nazo. La sivyo anaweza kupata madhara makubwa na hatimae hata kupata vilema au matatizo ya kudumu au hata kifo.
AINA ZA BATIKI
1. Batiki za kuchovya tie and dye2. Batiki za mshumaa
3. Batiki za kuprint
4. Batiki za kubabua(kublich)
5. Batiki za kufinyanga
BATIKI ZA KUCHOVYA (TIE AND DIE)
Ni aina ya nguo au vazi la asili linayotengenezwa kwa mikono kwa kuweka picha michoro na urembo mbalimbali.kwa hapa tanzania batiki soko lake kubwa na watu wengi wamejikita kufanya ujasiriamali huu unawaingizia kipato kikubwa na kuweza kumudu maisha yakitanzania
BATIKI ZA TIE AND DIE
Ni aina ya batiki ya kukunja mikunjo kwa kutumia mkono vilevile tie ni neon la kiingereza lenye maana ya funga na die ni neno la kiingereza lenye maana chovya hivyo basi ni batiki za kufunga mikunjo na kuchovya.
Malighafi
1. Cautic soda vijiko vitatu vya chakula2. Sodium hydrosulphet vijiko vitatu vya chakula
3. Rangi vijiko viwili hadi vitatu vya chakula.
VITENDEA KAZI:
Meza, kitambaa cha pambe, kalamu, uzi, sindano, mkasi, kamba, sufuria kijiko kikubwa, ndoo au beseni, jiko, vibanio, maski na gloves.
AINA ZA TIE AND DYE.
1. Kushona- chora mchoro wowote ushone, halafu vuta na uzi kwa nguvu.2. Kufanya- loweka kitambaa kisha tandika kwenye mkeka au nailoni, anza kuvuta kwa kufinyanga, kisha mwagia dawa.
3. Funga uzi na kamba-kunja mkunjo wowote funga na kamba, tumbukiza kwenye dawa.
4. Kutumia blichi (jiki)- tandika kitambaa kwenye meza halafu mwagia blichi yako uliyoiweka kwenye chupa na kutoboa mfuniko kwa ajili ya kutoa blich yako kama urembo
Baadhi ya hizi zinaweza kuchanganywa na kupata rangi kama ifuatavyo Red +blue=purple yellow+blue =green yellow+orange=chungwa green+red=brown=udongo=green dark orange +blue=combat-rangi ya jeshi
JINSI YA KUTENGENEZA.
2. Pima malighafi ya kwanza hadi ya tatu, weka vyote kwenye beseni.
3. Weka maji ya moto lita 2_3, koroga kwa dakika tatu,
4. Chovya kitambaa kwenye rangi acha kwa dakika 15 ili vipoe na kuingia rangi vizuri
5. anika kisha ukimaliza fua na upige pasi, tayari kwa kwenda sokoni
BATIKI ZA MISHUMAA
Mahitaji1. Vitambaa vya batiki
2. Sponji
3. Rangi vijiko 3
4. Sodium hydrsulphate vijiko 3 vya chakula
5. Caustic soda vijiko 3 vya chakula
6. Mshumaaa
7. Sufuria kubwa
8. Beseni
9. Meza
10. Jiko
11. Mti mrefu
VIFAA KINGA
- Gloves
- Miwani
- Viatu vigumu
- Brush
- Kiziba pua (barakoa)
- koti
A. Sodium
Kazi ya sodium hydrosulphate ni kuimarisha rangi isichuje kama itachanganywa na caustic soda.
Madawa haya yana kazi moja ila ikikossekana moja nyingine haifanyi kazi.
B. Mshumaa
Kazi yake ni kuweka nembo ktk nguo na ktk vitambaa kwa kutumia vibao au sponji zenye urembo wa tembo, twiga ,matunda au urembo wowote anaohitaji mtengenezaji.
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Weka mshumaa jikoni ili uweze kuyeyuka ukiyeyuka anza kukonga mshumaa kwenye kitambaa chako hakikisha unagonga mbalimbali kuruhusu kuweka mshumaa wa pili baada ya kuweka rangi ya kwanza acha mshumaa wako ukauke.2. Uwekaji rangi,Chemsha maji ya moto yachemke sana Kisha pima Lita 3hadi 4 pima caustic vijiko 3, pima sodium vujiko 3 changanya na maji Moto tia rangi kijiko 2-3
Baada ya hapo pima maji lita 6 ya baridi Kisha changanya na mchanganyiko wa madawa awali kusudi yapoe yawe vuguvugu.
Tumbukiza vitambaa vinee vya mita tatu kwa wakati mmoja na kuvigeuza geuza ili viingie rangi kwa dkk 20 Kisha suuza kwa maji ya baridi anika
3. Baada ya kukauka weka rangi ya kwanza chukua kitambaa chako chemsha mshumaa anza kugonga ua lingine kwenye kile kitambaa chemsha maji ongeza sodium hydrosulphate vijiko na rangi na caustic vijiko 3 koroga ongeza maji lita 5 anza kuchovya vitamba vyako viache kwa dakika 20 kisha suuza anika vikikauka nenda katoe mshumaa
Namna Ya Kutoa Mshumaa
Chemsha maji yachemke kabisa Kama ya kupikia ugali Kisha tumbukiza kimoja kimoja jikoni ili kuondoa mshumaa ktk kitambaa, Geuza kwa mti mrefu Kisha suuza kwa maji baridi anika kivulini na kabla hakijakauka vizuri piga pasi ili kuimarisha rangi.BATIKI ZA KUBABUA / KUBLICH
Katika kutengeneza batiki za kubabua tunatumia kutengeneza kwa kutumia jiki na kumwagia kwenye kitambaa au kutumia sponji kuweka ua ambalounalihitaji
Mahitaji
1. Kitambaaa2. Sodium/calcium hypochlorite vijiko 5
3. Maji nusu lita
4. Sponji au spry container
JINSI YA UTENGENEZAJI
1. Chukua chombo weka maji kisha weka sodium hypochlorite kisha tikisa au koroga hadi iyeyuke
2. Chukua kitambaa chako tandika chini au kwenye meza anza kunyunyiza yale maji yako yenye sodium hypochlorite kitaanza kubabuka ukimaliza 3. Chukua kitambaaa kifue na kianike
BATIKI ZA KUPRINT
Hizi ni batiki ambazo unatumia rangi na screen kwa ajili ya kutengeneza batiki hizi
Mahitaji
1. Vitambaa2. Rangi ya kuprint
3. Screen yenye michoro
4. Spatula ya kuwekea rangi kwenye screen
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Chukua kitambaa tandika kwenye meza au sakafu chukua screen yenye michoro anza kuweka alama sehemu unazohitaji kuweka2. Anza kuweka rangi kwenye screen huku ukifuta na kusambaza kwa kutumia spatula.
3. Baada ya hapo anika kivulini ikikauka chukua kitambaa laini weka juu ya batiki anza kupiga pasi ukimaliza tayari kwa kupeleka sokoni.
BATIKI YA KUPRINT
BATIKI ZA KUFINYANGA
Batiki hizi ni moja ya batiki rahisi kuliko zote hizi kwanza mchanganyiko wake unaandaliwa kama tie and dye za kuchovya.
MAHITAJI
1. Kitambaa
2. Sodium hydrosulphate vijiko 3
3. Caustic soda vijiko 3
4. Rangi vijiko 3
5. Maji lita 3
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Chukua vitambaa vyako weka kwenye maji kisha kamua viwe na umajimaji kwa mbali anza kufinyanga kwa kuvuta vuta kwa pamoja ukishamaliza2. Chukua sufuria weka jikoni weka maji lita 3 yakichemka ipua chukua chombo cha plastiki weka sodium hydrosulphate ,caustic soda na rangi kisha weka maji yale ya motokisha koroga ukimaliza
3. Anza kumwagia kidogo kidgo kwenye batiki zako ukimaliza acha zipoe kwa dakika 15 kisha kunjua kupata batiki anika kivulini ikikauka piga pasi fua tayari kwa kupeleka sokoni.
SABUNI YA UNGA
MAHITAJI:1. Soda ash 3.3kg.
2. LABSA 650mls.
3. Sodium sulphate 750grams.
4. Nansa 10grams.
5. STPP 750grams.
6. Optical Brightener 20grams
7. Perfume 20ml.
8. Rangi ukipenda{kadiria}
JINSI YA KUTENGENEZA:
1. Pima Soda ash 3.3kg, Mimina Sulphonic acid/LABSA 750grams kisha changanya vizuri.2. Mimina Sodium sulphate 750grams kisha changanya vizuri. Mimina Nansa 10grams kisha changanya tena vizuri.
3. Weka Sodium Trip polyphosphate {STPP} 750grams kisha changanya vizuri.
4. Weka Optical brightener 20grams kisha changanya tena vizuri.Weka rangi ukipenda {kadiria}
5. Weka perfume 20mls kisha changanya vizuri.Anika kivulini ikauke vizuri kisha weka kwenye vifungashio tayari kwa matumizi,
NB: Rangi ya sabuni ya unga si sawa na rangi ya sabuni ya maji na ya sabuni ya maji si sawa na ile ya Sabuni ya mche
SIAGI YA KARANGA
MAHITAJI1) Karanga kg 1/4
2) Asali kijiko 1.5 cha chakula
3) Peanut oil au mafuta yeyote kijiko 1 na nusu cha chakula
4) Chumvi 1/2 kijiko cha chai (k ama peanut zake hazijakua roasted na chumvi )
5) Chupa yenye mfuniko ya kigae ( kwa kuhifadhia peanut butter yako )
NAMNA YA KUTAYARISHA
1) Ondoa maganda karanga zako2) Osha vizuri then weka zikauke vizuri
3) Zioke katika oven dakika 30-35 minutes, moto 350F
4) Subir zipoe kidogo then mimina karanga katika blender ama food processor...saga dakika 1 acha kidogo saga hadi iwe laini
5) Ongeza asali, chumvi na mafuta saga hadi iwe laini... 6) Hifadhi katika chupa yako then weka kwenye friji tayari kwa matumizi.
LOTION AND CREAM
Malighafi
1. White oil lita 12. Stearic acid gramu 100
3. CSA gram 250
4. Cetal alcohol gram 250
5. Pola wax gramu 250
6. Lactic acid mls 100
7. Cetrimide mls 100
8. Salicylic acid gram 50
9. Methyl paraben gram 40
10. Propyl paraben gram 10
11. Glycerine ml 100
12. IPA -150-200 ml
13. Bee wax/ shea butter – gram 50 (sio lazima)
14. Pafyumu – mls 40
15. Kojic acid gram 10 -30 (sio lazima kwa ajili ya weupe zaidi)
KAZI ZA MALIGHAFI
1. CSA –uzito ,ngozi kung,arisha2. Cetal alcohol –uzito ,kungarisha
3. Pola wax –kiunganishi ,kufanya kuwa nyeupe ,emulsifier
4. Bee wax –kungarisha ngozi
5. White oil- kulainisha malighafi
6. Lactic acid –kutakatisha
7. Proply paraben –kuhifadhi
8. Methly paraben-kuhifadhi
9. Centrimide –kutoa michirizi kwenye ngozi
10. Salicylic acid –kutoa chunusi
11. Grycerine –kurainisha
12. IPA- kuondoa chunusi ,ubaridi
13. Stearic acid –kungaridha ngozi
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1. Weka maji lita moja jikoni pima centrimide iache iyeyuke weka salicylic acid iache iyeyuke kabisa koroga kisha ipua weka pembeni2. Chukua sufuria nyingine weka white oil (unaweza kuweka alovera oil /mafuta ya alizeti) kisha weka stearic acid ikiyeyuka pima CSA weka kwenye sufuria, weka cetal alcohol iache iyeyuke vizuri weka pola wax.
3. Weka menthly parabene na propyl paraben (ukiwa na bee wax unaweka wakati huu)
4. Chukua maji lita mbili weka kwenye mchanganyiko ule wa mwanzo kwenye beseni
5. Zima jiko chukua mchanganya wa pili anza kuchanganya na mchanganyiko wa mwanzo kisha koroga weka maji kisha endelea kukoroga vizuri
6. Weka IPA na grycerine weka kisha koroga vizuri
7. Weka lactic acid kisha koroga weka pafyumu
Kumbuka
1. Rangi unaweka kwenye white oil2. Vitamin c gram 50 /mls 50 unaweka kwenye mchanganyiko wa kwanza
3. Ukitaka iwe cream acha maji lita 8 ukitaka lotion weka maji hadi lita 15
LOTION YA PARACHICHI
Lotion hii kwaajili ya kuifanya ngozi iwe ya asili( Natural soft skin).Na haichubui hata kidogo.
MAHITAJI
1. Parachichi zilizoiva vizuri- 3 au 42. Almond oil - 100mls/kichupa 1
3. Vitamin E - matone 4 / ya vidonge
4. Shea butter - mls 250
5. Aloe vera velly - 50mls
6. Rose water - kijiko 1
7. Preservative - kijiko 1 cha chai
UTENGENEZAJI
1. Chukua parachichi menya kisha saga kwenye blenda mpaka upate juice nzito na laini kabisa. (smooth juice).2. Kisha yeyusha shea butter na itie kwenye rojo au juice la parachichi na ukoroge vizuri mchanganyiko huo.
3. Baada ya hapo tia Almond oil kichupa kimoja au 100 mls na kisha endelea kukoroga.
4. Tia Aloe vera gelly 50mls kisha endelea kukoroga.
5. Chukua vitamini E (for skin) dondoshea matone 4 au unaweza tumia ya vidonge 4 na ukoroge vizuri.
6. Tia rose water kijiko 1 na ukoroge.
7. Weka essential oil (perfume) uipendayo kijiko 1 na ukoroge vizuri.
8. Mwisho utaweka Organic preservative ili kuifanya lotion yako ikae kwa muda mrefu bila ya kuharibika.
9. Weka katika vifungashio tayari kwa matumizi.
MATUMIZI:
Lotion hii ni kwaajili ya kung'arisha na kuifanya ngozi iwe soft.(soft natural skin).-Lotion hii ni nzuri kwa wenye ngozi kavu itawafanya ngozi zao kuwa na unyevu nyevu. (very soft).
LOTION YA LIMAO(LEMON
Lotion hii ni nzuri kwa wenye sura au ngozi yenye mafuta.Huondoa chunusi, mabaka na kuifanya ngozi yako ipendeze.MAHITAJI
1. Micro wax -½ kg2. White oil - ½ au 1 lita
3. Paraffin wax - ½ kijiko
4. Rangi - kijiko 1 cha chai
5. Perfume - kijiko 1
6. Limao – 10
7. Flavour(lemon) -Vijiko 3 vya chai
NB: PARAFFIN WAX - Unaweza kuongeza kama utahitaji lotion yako isiwe nzito.
UTENGENEZAJI
1. Chukua sufuria kubwa ya maji weka jikoni.Maji yakianza kuchemka chukua sufuria nyingine ikalishe juu ya maji.(double boiler).2. Weka micro wax kisha iache iyeyuke,
3. Weka parrafin wax kisha nayo iache iyeyuke kabisa.
4. Kisha weka white oil na baada ya hapo anza kukoroga taratibu kwa dakika kadhaa.
5. Kamua malimao yako upate juice.Kisha mimina juice hiyo ndani ya mchanganyiko wako na ukoroge vizuri.
6. Weka rangi 10 gm au kijiko 1 na ukoroge kwa dk 3 hadi 5
7. Weka ladha/ Flavour vijiko 5 vya chai
8. Weka Perfume ya Lemon na koroga vizuri.
9. Weka preservative kijiko 1 cha chai na ukoroge vizuri.
10. Fungasha na upeleke sokoni.
WHITENING & SOFTENING BODY SERUM
Hii ni kwaajili ya kung'arisha.MAHITAJI
1. Mafuta ya nazi(pure) - 50mls2. Vitamin E - vijiko 2
3. Almond Oil- vijiko 2
4. Rose water - vijiko 4/ 40mls
5. Preservative- 10 mls
6. Carot - 1 au 2
7. Manjano - kijiko 1 cha chakula
8. Maziwa - 30mls/ vijiko 3
9. Alóe vera gelly - 10mls
10. Gryceline - nusu kijiko/ 5mls
11. Asali - kijiko 1
12. Perfume - 10 mls
HATUA ZA UTENGENEZAJI
1 Andaa chombo chako(Bakuli) safi na kavu. Weka Almond oil, Vitamin E, na Gryceline kisha changanya vizuri mchanganyiko wako kisha weka kando(pembeni).2 Chukua chombo kingine (Bakuli) kisha weka maziwa, asali, rose water na Aloe vera gelly kisha koroga vizuri mpaka vichanganyikane vizuri.
3 Kwenye mchanganyiko wa hatua ya pili(wa maziwa) tia manjano, preservative, kisha koroga vizuri na weka pembeni.
4 Chukua mafuta ya nazi ya asili kabisa ambayo hayajachakachuliwa yaweke katika sufuria kisha weka jikoni yapate moto alafu tia karoti iliyosagwa kaanga mpaka karoti ibadilike rangi iwe ya brown na mafuta yawe ya Orange. Kisha zima moto na epua.
5 Chukua bakuli lenye maji tumbukiza sufuria yenye mchanganyiko wa mafuta ya nazi na karoti itumbukize ielee uku mfuta yakipoa ila yasipoe sana.
6 Chukua kitambaa safi chuja mafuta ya nazi yatengane na mafuta ya karoti.
7 Kisha chukua bakuli lenye Almond oil, Gryceline na vitamin E mimina kwenye mchanganyiko wa mafuta ya nazi na karoti kisha koroga vizuri kwa dk 5 hadi 10.
8 Chukua bakuli lenye mchanganyiko wa maziwa, asali, rose water na Aloe vera gelly changanya au mimina kwenye bakuli kenye mchanganyiko wa awali( hatua ya saba) kisha koroga vizuri kwa dk 10-15.
9 Kisha chukua Essntal perfume tia alafu koroga vizuri.
10 Baada ya hapo weka katika vifungashio tayari kwa matumizi.
COFFEE BODY SCRUB (1kg )
Sasa hii ni jinsi ya kutengeneza coffee scrub bila kutumia sugar (sukari) endapo utataka kutengeneza emulsifying coffee sugar scrub maji hayahusiki. Hivyo hatutakuwa na kitu kinaitwa water phase.MAHITAJI
1. (Waterphase) 2. Maji 820g4. Cap B 100g 5. sles 20g
3. Xgum 6g
Weka vyote kwenye sufuria ya stainless steel .
MAHITAJI
(Oil Phase)1. Stearic acid 5g 2. Cetyl alcohol 30g
3. Coconut oil 20g 4. Salicylic acid 1.5g
5. Coffee powder 2g 6. Potassium sorbate 5g
Weka vyote kwenye sufuria ya pili kasoro (usiweke salicylic acid coffee powder potassium sorbate.
JINSI YA KUTENGENEZA.
1. Chukua sufuria kubwa weka maji kiasi na weka jikoni.2. Kisha chukua sufuria mbili ndogo zenye malighafi na uziweka ndani ya sufuria kubwa jikoni zielee katika maji yanayochemka.
3. Weka vipima joto katika sufuria zenye malighafi hakikisha hazigusi sufuria.
4. Joto likisoma 75°c zima jiko na chukua malighafi za sufuria moja uchanganye na za kwenye sufuria nyingine kwa pamoja.
5. Kisha weka kwenye blenda na uanze ku blend. Joto likipungua weka botanical powder ( Coffee powder) na uchanganye vizuri kwa blenda.
6. Joto likishuka zaidi chini ya 40°c au iwe nyuzi 40°C utaanza kuweka potassium sorbate na salicylic acid na uchanganye vizuri kwa kutumia kijiko au spatula na sio blenda.
Mpaka hapo Scrub itakuwa tayari, utaipack vizuri tayari kwa matumizi.
SUGAR SCRUB
(Mfano wa Pili wa Scrub)Ukisikia emulsifying, maanake hazihusishi maji (hakuna water phase / hakuna malighafi zenye asili ya maji. Unatengeneza kilo moja ambayo ni sawa na gram 1000 za scrub
MAHITAJI
1. Cocoa butter 200g 2. Mango butter 100g3. Cetyl alcohol 100g 4. Ewax 100g
5. Avocado oil 440g 6. Orange oil 40g
7. Germa 10g 8. Lemon essential oil 30g
9. Sukari 1000g
Note: Sio lazima itumie butter nilizotumia na mafuta niliyotumia unaweka kuweka mengine kulingana na matakwa yako scrub isaidie nini kwenye ngozi.
UTENGENEZAJI
1. Weka vyote kwenye sufuria kasoro essential oil germa na sukari2. Bandika sufuria yenye maji kiasi kubwa kuliko ya mwanzo jikoni. Tumbukiza sufuria yenye malighafi iwe inaelea. Acha malighafi ziyeyuka dakika 20 (uwe na saa), kisha epua
3. Peleka kwenye freezer acha igande mpaka uone Tabaka limejitengeneza dakika 20 .
4. Changanya kwa kutumia blender /hand mixer spidi kubwa hadi uone imekuwa nzitonzito(heavy) na laini(soft)dakika 10
5. Weka essential oil ,germa kisha changanya vizuri kwa kutumia kijiko kisafi cha plastic au spatula na sio hand mixer.
Pack kwenye vifungashio vyako tayari kwa matumizi au kupeleka sokoni.
SCRUB YENYE EXFOLIANT ZAIDI YA MOJA NATUMIA EXFOLLIANT ZAIDI YA MOJA . PIA SITATUMIA MAJI (SCRUB ITAKUWA EMULSIFYING )
EXFOLIANT NINAZOCHAGUA NI manjano na mchele. Nitahakikisha niko na fine powder zakeMahitaji kutengeneza kilo moja ya scrub
1. Shea butter 100g 2. Cocoa butter 200g
3. Cetyl alcohol 100g 4. Ewax 100g
5. Olive Oil 440g 6. Orange Oil 40g
7. Germa 10g 8. Clove essential Oil 30g
9. Manjano 500g 10. Mchele 500g
UTENGENEZAJI
1. Chukua sufuria kubwa weka maji kiasi na weka jikoni.2. Chukua sufuria nyingine weka malighafi zote isipokuwa exfoliant, Germa(preservative), na essential oil.Hivi havita ingia jikoni.
3. Weka sufuria hiyo yenye malighafi ndani ya maji kwenye sufuria kubwa iliyopo jikoni na acha ielee juu ya maji mapaka malighafi ziyeyuke.(dk 20)
4. Epua mchanganyiko wako na weka katika freezer, mchanganyiko ugande na kutengeneza tabaka kisha utaitoa.(huchukua dk 20)
5. Kisha utaitoa katika freezer na uta blend mpaka mchanganyiko wako uwe mzito na laini.(dk 10)
6. Ukishakuwa laini utaweka zile malighafi zingine ambazo ni Germa, essential oil, na exfoliant yako.- Changanya vizuri kwa kutumia kijiko cha plastic au Spatula na sio mixer au blenda tena.
Mpaka hapo itakuwa tayari, weka kwenye vifungashio, weka lebo na peleka sokoni.
NATUMIA EXFOLLIANT ZAIDI YA MOJA PIA NITATUMIA MAJI SCRUB HII ITATAKUWA NA VIPENGELE VIWILI WATERPHASE NA OIL PHASE EXFOLLIANT
NILIZOCHAGUA KUTUMIA ni nyanya na tango Hakikisha una unga wa nyanya na tango MAHITAJI (kutengeneza kilo moja) waterphase (kipengele cha maji na malighafi zenye asili ya maji)1. Maji 820g 2. Xgum 6g
3. Cap B 100g 4. Sles 20g
Weka vyote kwenye sufuria ya stainless steel kipengele cha pili oil phase mahitaji.
1. Citric acid 5g 2. Cetyl alcohol 30g
3. Coconut oil 6g 4. Salicylic acid 1.5g
5. Tango 8g 6. Nyanya 8g
7. Potassium sorbate 5g
Weka vyote kwenye sufuria ya pili kasoro salicylic acid exfoliant zako ambazo ni tango na nyanya preservative yako ambayo ni potassium sorbate.
JINSI YA KUTENGENEZA
1. Kwanza kabisa hakikisha una exfolliant zako kwenye mfumo wa unga unga (powder)2. Weka malighafi zote zenye asili ya maji katika sufuria moja.
3. Kisha chukua malighafi zenye asili ya mafuta (Oil phase) na weka katika sufuria nyingine.
4. Kisha utachukua sufuria nyingine kubwa utaweka maji kiasi kidogo na utabandika jikoni.
5. Kisha utatumbukiza sufuria zako mbili zenye malighafi ndani ya sufuria kubwa lenye maji.
6. Weka vipima joto ndani ya hizo sufuria zenye malighafi( Hakikisha hazigusi sufuria)
7. Joto likifika 75°C ipua na changanya malighafi zako katika chombo kimoja.
8. Joto likiwa chini ya 40°C utaweka Exfolliant na preservative na utachanganya tena vizuri.
Mpaka hapo Scrub yako itakuwa tayari.Weka katika vifungashio, weka Lebo na upeleke sokoni.
Active ingredient: hapa tuna maanisha zile kemikali ambazo zinachangia kwenye kutibu matatizo ya ngozi. Kwa mfano SALICYLIC ACID hutibu chunusi.
KAZI ZA BAADHI YA EXFOLIANT:
1. NYANYA - Hutumika kuondoa au kupunguza makunyanzi au mikunjo usoni au katika ngozi.- Hulinda ngozi dhidi ya mionzi ya jua.
2. TANGO - Kuondoa chunusi na madoa.
3. COFFEE - Huondoa michirizi.
- Kufanya ngozi kuwa laini.
4. MANJANO - Kung'arisha ngozi na kuondoa makovu.
5. MCHELE - Husaidia sana kwa watu wenye ngozi za mafuta (Hubalance mafuta yaliyozidi)
- Hung'arisha
- Kuleta rangi moja.
Kwahyo utachagua Exfolliant yyte kulingana na mahitaji yako.
TILES & SINK CLEANER
Malighafi
1. Sless ¼ kg2. Hydrocloric acid 6 lt
3. Rangi njano kiasi
4. Perfume 50 MLS
5. Maji Lita 20
UTENGENEZAJI:
1. Weka sless katika ndoo yenye ujazo wa zaidi ya Lita 20 kisha koroga ongeza chumvi kidogo Kama gram 150 tu ili isaidie kuyeyusha sless kisha koroga vizuri Hadi kupata creamy na Kisha tia maji kidogo kidogo huku ukikoroga kuelekea upande mmoja, endelea kuongeza maji kidogo kidogo Hadi maji yaishe huku unakoroga.
2. Weka hydrocloric acid yote kidogo kidogo Hadi iishe huku unaendelea kukoroga .
3. Chukua rangi iloweke kando kisha koroga na itie kidogo kidogo kadiria rangi isizidi iwe kiasi kidogo tu.
4. Mwisho tia pafyum koroga vizuri na acha kwa saa 24 Kisha fungasha peleka sokoni.
5. Mtumiaji ahakikishe anavaa gloves na miwani wakati wa kutumia hii dawa ya kunga' risha sink , rashia eneo husika kisha sugua kwa sabuni baada ya dakika 60-90.
Naamini makala hii itakuwa imekusaidia sana katika kujifunza mambo mbalimbali ambayo yataharakisha safari yako ya mafanikio. Ninakusihi ufanyie kazi yale uliyojifunza kwa bidii ili upate matokeo makubwa zaidi. Kumbuka kuwa una uwezo mkubwa sana ndani yako na kama ukiamua kuufanyia kazi basi hakuna kitu ambacho kitakuzuia. Nakutakia mafanikio katika ndoto yako
Ni mkufunzi na mshauri katika Utengenezaji wa sabuni za aina zote, kwa ufanisi mkubwa kwenye vikundi mbalimbali ndani ya Tanzania na watu binafsi nafundisha.
Jumanne Mwita
JF-Expert Member
- Thread starter
- #3
nenda SIDO yapo
mzalendo namba moja
JF-Expert Member
Unforgettable
JF-Expert Member
ubarikiwe mpaka ushangae
asubuhi sana
JF-Expert Member
Saf
Similar Discussions
- Jifunze namna ya kutengeneza sabuni za maji, kufulia, shampoo, sabuni za miche na chooni
- Started by Jumanne Mwita
- Replies: 33
No comments:
Post a Comment