NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amekuwa akipasua kichwa namna ya kuweza kutatua tatizo la mabao ya mipira iliyokufa jambo ambalo limekuwa tatizo kwa timu hiyo kwa hivi karibuni.
Jana Yanga ilipoteza kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Rivers Niger na kumaliza mwendo katika hatua ya awali.
Ni safu ya ulinzi pamoja na viungo wa Yanga walikuwa wamekaa kikao ili kujadili namna ya kuweza kuondoa hali hiyo ya kufungwa mabao kwa mipira ya adhabu.
Taarifa kutoka kwa moja ya viongozi wa Yanga ilieleza kuwa Nabi hafurahishwi na kuona timu hiyo inafungwa mabao yanayotokana na mipira ya kutengwa jambo ambalo linampasua kichwa.
"Baada ya mchezo dhidi ya Rivers United lile bao lilifanya Nabi aweze kukaa na wachezaji na kuzungumza nao kuhusu makosa ya mara kwa mara, kikubwa anahitaji umakini na hilo litakuwa na mabadiliko makubwa," amesema mtoa taarifa hiyo.
Moja ya mabeki wa kutegemewa ndani ya Yanga ambaye ni nahodha, Bakari Mwamnyeto alisema kuwa kumekuwa na tatizo katika mabao wanayofungwa kutokana na mipira ya kutengwa jambo wanalolinfanyia kazi ili lisijirudie.
"Makosa kwa upande wa mabao ambayo tunafungwa ikiwa ni yale ya kona na faulo ni moja ya mambo ambayo hatupendi kuona yanatokeo hivyo kwa wakati huu tunazidi kujiweka sawa ili kupunguza makosa,".
Mchezo ujao wa Yanga ni dhidi ya Simba ambao ni maalumu kwa ajili ya ufunguzi wa ligi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 25.
No comments:
Post a Comment