Guardiola Asikitikia Sare ya Man City - KIVUTIO

Breaking

daily job opportunities, sports, life psychology, scholarship, education notes and information and health

Monday, September 20, 2021

Guardiola Asikitikia Sare ya Man City

 

KOCHA wa Man City, Pep Guardiola amesema kuwa anajisikia vibaya kuona timu yake imeshindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Southampton.

Man City na Southampton, zilivaana juzi kwenye mchezo wa Ligi Kuu England ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.

Hivi karibuni, Pep Guardiola alikuwa akitumia nguvu kubwa kuwashawishi mashabiki kuhudhuria uwanjani kwenye mchezo huo lakini timu yake ikaambulia sare.

Guardiola amesema ni jambo baya sana kwake kuona wanapata sare kwenye mchezo huo, lakini anataka mashabiki wake wasikate tamaa kwani watashinda michezo ijayo.

“Sikusema jambo lolote baya kwenye mchezo dhidi ya Leipzig, nilisema kuwa tunacheza mchezo mgumu sana dhidi ya Saint’s na tunahitaji mashabiki uwanjani.

“Sikusema lolote kuhusu nani alikuja uwanjani na nani hakuja, sijawahi kusema hivyo kwenye maisha yangu ya soka.

“Ukweli ni kwamba kocha yoyote anataka kuona mashabiki wengi uwanjani, lakini leo sijafurahishwa na matokeo kwa kuwa sikupenda hali hii itokee.

“Kila siku nimekuwa nikijisikia vibaya ninapoona mambo hayaendi vizuri lakini nataka kuwahakikishia mashabiki kuwa waje uwanjani, leo hatukucheza vizuri hata kidogo huko mbele tutakuwa bora,” alisema Guardiola raia wa Hispania.

MANCHESTER, England


No comments:

Post a Comment